• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi wilayani Bukombe.

Imewekwa: August 28th, 2017

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula (MB) amefanya ziara ya siku moja wilayani Bukombe na kutembelea idara ya Ardhi na Maliasili namna inavyofanya kazi kwa kutumia mfumo wa kieletroniki.Katika ziara hiyo Mhe Naibu Waziri ametaka kufahamu Halmashauri imeshatoa Hatimiliki ngapi? kulingana na malengo yaliyotolewa na Wizara ya Ardhi kwa Halmashauri na kwanini malengo hayajafikiwa? aidha pia Mhe Naibu Waziri ametaka kufahamu makusanyo ya kodi ya Ardhi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ni kiasi gani? na je lengo ililokuwa limepangwa limeweza kufikiwa? vilevile ametaka kufahamu endapo Halmashauri ina migogoro ya ardhi na utatuzi wa migogoro hiyo umefanyika?. 

Afisa Ardhi Mteule  Ndugu  Joseph Kimambo amejibu kuwa Halmashauri imeandaa jumla ya hatimiliki 54 kutokana viwanja vingi katika mji wa Ushirombo kutokamilishwa upimaji wake ambavyo vipo kwenye hatua ya upimaji wa awali, pia upungufu wa wataalamu wa kusaidia zoezi la umilikishwaji mfano ukosefu wa mchora ramani husababisha kuchelewesha zoezi la maandalizi ya Hati. Ameongeza pia kuwa gharama kubwa za kuandaa hatimiliki zinawafanya wananchi wengi kushindwa kumudu kuandaliwa hatimiliki, katika kuhakikisha Halmashauri inaandaa hatimiliki za kufikia lengo, kwa kushirikiana na Mwananchi imeingia ubia na makapuni mawili ya ya upimaji ambayo ni Geolink Survey Ltd na Amboni Land Consult Ltd ili kukamilisha upimaji wa viwanja na hatimiliki kuandaliwa. Pia Halmashauri imetenga katika bajeti (PE) ya mwaka wa fed 2017/2018 kwaajili ya kuajiri wataalamu wa fani ya Ardhi ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wateja.

Katie kujibu swali la makusanyo ya Ardhi, Afisa Ardhi mteule amesema malengo yaliyotolewa na Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Halmshauri ya wilaya ya Bukombe katika mwaka wa fedha 2016/2017 ni kukusanya kiasi cha Tsh.100,000,000 hadi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri imeweza kukusanya kiasi cha Tsh.26,850,000 sawa na 25% ambayo ni robo ya lengo la makusanyo yote,Hali hii imesababishwa na ukosefu wa fedha za uhamasishaji ambao pia unachangiwa na kutorejeshwa kwa 30% ya fedha za kodi ya Ardhi zinazotumwa Wizara ya Ardhi ambapo hadi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri imekusanya kiasi cha Tsh.26,147,208 kwenye akaunti ya Wizara ya Ardhi na inadai kiasi cha Tsh.7,844,165.5 mrejesho wa 30% kwenye idara na tayari fedha za kuomba mrejesho wa 30% kutoka Wizara ya Ardhi.

Migogoro ya Ardhi ndani ya wilaya ya Bukombe inatokana na madeni ya fidia yaliyodumu tangu Halmashauri inaanzishwa mwaka 1995,Halmashauri imeshughulikia migogoro hiyo kwa wananchi wanaodai fidia kwa kuzingatia hali ya upatikanaji wa Mapato na hadi kufikia mwezi julai mwaka 2017 deni la fidia lilikuwa Tsh.228,816,340 ambapo Halmashauri imepunguza deni hilo kwa kulipa kiasi cha Tsh.10,366,340 kutoka kwenye mapato ya ndani (own source). amejibu Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mhe.Josephat Maganga.

Pichani Naibu Waziri wa Ardhi Mhe.Josephat Maganga,Nyumba na Maendeleo ya Makazi akitaka ufafanuzi wa Rejesta ya kumbukumbu ya usimamizi na utawala wa Ardhi.

Pichani ni Naibu Waziri Mhe.Angelina Mabula na Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mhe Josephat Maganga wakielekea ofisi ya Ardhi na Maliasili ya Halmashauri ya wilaya ya Bukombe.

Pichani ni Naibu Waziri wa Archi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula akitoa maagizo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.

Mhe Angelina Mabula ameitaka Halmashauri kuhakikisha inaimarisha mfumo wa kukadiria kodi ya Ardhi kwa kuweka Rejesta ya kumbukumbu ili kurahisisha shughuli za usimamizi na utawala wa Ardhi, Pia amesisitiza wananchi waelimishwe umuhimu wa kuendeleza viwanja na mashamba pori kwa mujibu wa sheria ya Ardhi No 4 ya mwaka 1999 ya viwanja kuendelezwa ndani ya siku 3 tangu vilipogawiwa kwa waombaji. Na kuhakikisha lengo lilipongwa la Hatimiliki 500 linafikiwa sambamba na upimaji viwanja ndani ya wilaya. Amesisitiza pia "Hakikisheni mnatambua na kutangaza maeneo yaliyoiva kimipango miji kwa kuwashirikisha wananchi,pia utambuzi wa maeneo ya umma ufanyike na maeneo hayo yapimwe na kupewa hati" amesema Naibu Waziri.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya 3 kwa mwaka 2024/2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa