• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri yatakiwa kutoa elimu juu ya utekelezaji wa sheria mpya ya umiliki wa ardhi

Imewekwa: August 12th, 2020

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula (MB) ameitaka halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kutoa elimu kwa wananchi  kupitia vyombo vya habari na mikutano ya hadhara juu ya sheria Na 8 ya fedha ya mwaka 2020 ya umiliki wa ardhi. Sheria hiyo ilianza kutekelezwa tarehe 1 Julai 2020 inayowataka wananchi kumilikishwa ardhi ndani ya siku 90 baada ya mchoro kuwa umeidhinishwa vinginevyo watakutana na limbikizo la kodi.

“wananchi wapewe elimu juu ya sheria mpya inayowataka wananchi ambao maeneo yao yalishapimwa na kidhinishwa  kuomba umiliki wa viwanja vyao.”

Mabula ameyasema hayo leo tarehe 12 Agosti, 2020 wakati wa ziara yake  Wilayani Bukombe.

Aidha ameitaka Idara ya Ardhi kuhakikisha inapima maeneo yote ya Umma kama masoko, vituo vya polisi, stendi, ofisi za zima moto, hospital, shule na maeneo mengine ambayo ni mali ya Umma ili kuepusha migogoro.

“Lazima maeneo yote ya Umma yawe yamepimwa na yamemilikishwa ili kuepusha migogoro ya taasisi na wananchi.”

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said Nkumba amesema  Idara ya Ardhi inachangamoto ya upungufu wa watumishi katika kada za Afisa Ardhi Mteule 1, Mtunza kumbukumbu 1, Maafisa Mipango Miji 2, Mrasimu Ramani 1 na Wathamini 2. Hata hivyo  halmashauri kupitia Ofisi ya  Utumishi inaendelea kuomba vibali vya kuajiri watumishi hao.

Kwa upande wake Afisa kilimo Umwagiliaji na Ushirika Wilaya (DAICO) Joseph Machibya kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji  amesema Halmashauri  iliwekewa lengo la kukusanya jumla ya shilingi 300,000,000.00 kutokana na tozo mbalimbali za ardhi. Hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2020 halmashauri ilifanikiwa kukusanya jumla ya shilingi 110,547,997.00 sawa na asilimia 36.67 ya lengo. Aidha changamoto kubwa iliyopelekea kutofikia  ni kutokuwa na watumishi wakutosha pamoja na vitendea kazi.

Hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ilipokea fedha kiasi cha shilingi 123, 000,000.00 kutoka wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya upimaji wa viwanja 2,000 katika maeneo ya Msimila na Uyovu. Hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2020 jumla ya viwanja 2,672 vimemepimwa sawa na asilimia 133.6 ya lengo.

Regina Ndungulu akipokea hati ya umiliki wa Ardhi kutoka kwa Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula.


Baadhi ya washiriki wa kikao.


Wananchi wakiwa wameshikilia hati miliki nyuma ya Naibu waziri wa Ardhi.






Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya 3 kwa mwaka 2024/2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa