• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Shule Mbili zatunukiwa Hati ya Pongezi

Imewekwa: July 16th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said Nkumba tarehe 15 Julai, 2020 amezipatia shule mbili hati ya pongezi kwa kuwa washindi wa kwanza katika mashindano ya Usafi wa Mazingira kwa ngazi za taasisi yaliyofanywa na Wizara ya Afya  Mei na Juni, 2020. Hati hizo zimetolewa katika kikao kazi cha mapitio ya shughuli za kampeni ya kitaifa ya Usafi wa mazingira.

Nkumba amempongeza  Mkuu wa  Shule Sekondari  Businda na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ibamba  kwa kupata  hati hizo katika mashindano ya ndani ya Wilaya .Pia amewapongeza Wahandisi pamoja na  Watendaji wa Kata kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa  matundu ya vyoo bora katika taasisi  za serikali.

 Afisa afya kutoka ofisi ya  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe William Sango amesema halmashauri ya Wilaya ya Bukombe wa mwaka kwa fedha 2019/ 2020 imepokea jumla ya Shilingi 455,000,000/= kutoka  program ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ( SRWSS) inayofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa mfumo wa (P4R) Lipa Kulingana na Matokeo kwa ajili ya Kukarabati au kujenga miundombinu ya vyoo,  mifumo ya maji, kuweka mifumo na vifaa vya kunawia mikono, kuweka vifaa vya kutakasa mikono na kujenga au kukarabati mabafu katika wodi ya wazazi.

Aidha Nkumba amewataka watendaji wa kata kuhakikisha wanasimamia  vizuri ujenzi wa miradi ya vyoo inayotekelezwa kwa fedha za program ya maji na Usafi wa mazingira Vijijini ili Wilaya iweze kupata fedha nyingi zaidi na kuondoa changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo.

Naye Mkurugenzi Mtendajiwa wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Dionis Myinga, amewataka watendaji wa kata kuhahikisha wanawashirikisha  wananchi katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa vyoo bora  inayotekelezwa na program ya maji na usafi wa mazingira.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Uyovu  Bartazali Bundala  kwa niaba ya Watendaji wa Kata amesema  wapo tayari kupambana na changamoto ya ukosefu wa matundu ya vyoo katika kata zao kwa kutumia sheri ya Usafi wa  Mazingira ili kuhakikisha kaya zote zinakuwa na vyoo bora Kwa ajili ya kujiepusha na magonjwa ya kuharisha yanayopelea vifo hususani katika nchi zinazoendelea.

Washiriki wa kikao kazi hicho walikuwa ni baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa halmashauri pamoja na watendaji wote wa kata.



Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said Nkumba (mwenyeshati la kitenge katikati) akisikiliza mada.




Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe Paul Cheyo  akichangia mada



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukomba  Dionis Myinga akichangia mada.



Mtendaji wa Kata ya Uyovu  Petro Mkude akipokea Hati  pokenzi kwa niaba ya Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Ibamba.


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa