• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

TAS - Bukombe yafanya kikao cha kimkakati

Imewekwa: September 22nd, 2018

Chama cha watu mwenye Ualbino Tanzania (TAS) chini ya mradi jumuishi wa watu wenye ualbino unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la Lilliane Foundation kimefanya kikao cha kimkakati  katika ukumbi wa mikutano wa makuti Wilayani Bukombe kwa ajili ya kujadili mipango itakayowezesha  upatikanaji wa huduma bora za bima ya afya (CHF), mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) unavyoendeshwa, upatikanaji wa mikopo kutoka Halmashauri na utoaji wa elimu kwa watu wenye ualbino katika shule za serikali na za watu binafsi.

Akifungua  kikao hicho Mwenyekiti wa TAS Ndg. Ida Saka ameomba ushirikiano  wakutosha kutoka kwa wataalamu wa Halmashauri  ya Wilaya ya Bukombe ili waweze kufanya kazi na kufikia malengo ya mradi yaliyokusudiwa ikiwa ni kupata ufahamu na kujadili  namna ambavyo watu wenye ualbino watakavyoweza kunufaika.

Naye Mratibu wa mfuko wa bima ya afya ya msingi (CHF) Ndg.  Revocatus F. Nyamweni amewaomba walemavu wa ngozi kuhakikisha wanajiunga na  mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF)  ili kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua na kuongeza wingi wa upatikanaji wa huduma za afya, Nyamweni amesema hayo wakati akiwasilisha mada ya mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) kwa wajumbe wa kikao hicho.

Aidha  Mratibu wa  mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF)  Ndg. Prisca M.Lyimo amesema mradi wa TASAF umelenga kuziwezesha kaya maskini  sana kwa watu wote wenye ualbino na wasio albino. Pia mradi  unatoa elimu kwa walengwa namna bora ya kutumia fedha wanazowezeshwa ili kujikwamua kiuchumi. "Mradi wa kunusuru kaya maskini ni wa watu wote kutoka kaya maskini  sana bila kuangalia familia hizo kama zina ulemavu wa ngozi" 

Ndg. Vumilfa Mchwapaka ametoa ushauri kwa watu wenye ualbino kuhakikisha wanaunda vikundi  vya kuweka na kukopa ili waweze  kunufaika na  asilimia mbili (2%) ya mkopo wenye riba nafuu kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.

Naye Afisa elimu maalum Ndg. Japhary Buya amewahakikishia viongozi wa TAS pamoja na wataalamu kuwa shule ya   msingi  Ushirombo inausalama wa kutosha hivyo wawapeleke watoto  wenye ualbino shuleni kwani kupata elimu ni haki yao. Ndg. Buya alisema "Mpaka sasa tumeishapokea  mafuta,karatasi maalumu za wasioona na mashine za kuandikia maandishi ya wasioona na kofia kwa watoto wenye ualbino kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI". Pia aliendelea kusema kuwa watoto wenye ualbino wanapewa karatasi zenye maandiko makubwa “Enlarged print”  na pia wanapewa muda wa nyongeza vakati wa mitihani kwa ajili ya kuwaboreshea mazingira ya ujifunzaji.

Katika kuhitimisha Kikao hicho  kaimu Mwanasheria wa Halmashauri Ndg Stephano Bugalama  amewaalika viongozi wa TAS kutembelea ofisi ya Mwanasheria wa Halmashauri ili kupewa miongozo  na namna ya kutengeneza Katiba inayozingatia sheria mama ya uundaji vikundi kwa ajili ya kupata fulsa nzuri ya kupata mikopo kama vikundi vingine.


Mwenyekiti wa Chama Cha Watu wenye Ualbino Wilayani Bukombe Bi.Ida Saka akifungua kikao.


Afisa Elimu Maalumu Ndg Japhary Bayu akitoa mada wakati wa kikao mkakati hicho.


Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho.



Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya 3 kwa mwaka 2024/2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa