• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wawezeshaji TASAF wapatiwa mafunzo ya Uhakiki wa kaya kwa kutumia kishikwambi

Imewekwa: July 1st, 2020

Wawezeshaji wa TASAF wamepatiwa mafunzo ya siku mbili ya kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III) kuhusu Uhakiki wa Kaya za Walengwa wa Mpango kwa kutumia kishikwambi ili kuwajengea uelewa wa pamoja wa namna zoezi  la uhakiki wa walengwa litakavyofanyika kwenye ngazi ya Mamlaka ya Eneo la Utekelezaji.

Akisoma hotuba ya ufunguzi  wa mafuzo hayo Afisa Ufuatiliaji TASAF Makao Makuu Moris Momba amesema

“Wakati wa Uzinduzi wa Kipindi hiki cha Pili, Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli aliagiza  kwamba kabla ya shughuli zozote za Kipindi cha Pili kuanza, uhakiki wa walengwa ufanyike kote nchini ili kuondoa kaya zote za walengwa ambazo zimepoteza sifa”

Momba aliendelea kusema kuwa  Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III) utekelezaji wake utafanyika  nchini katika maeneo ambayo hayakupata fursa hiyo katika Kipindi cha Kwanza cha utekelezaji wake ambacho kimekamilika.

Aidha amesema mkazo mkubwa katika Kipindi cha Pili utawekwa katika kuwezesha Kaya zitakazoandikishwa kwenye Mpango kufanya kazi ili kuongeza kipato na kitahakikisha kwamba huduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa ili kutoa huduma na kuendeleza rasilimali watoto hususan katika upatikanaji wa elimu na afya. 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Dionis Myinga amewataka wawezeshaji hao kuhakikisha wanakuwa waadilifu wanapokwenda kufanya kazi ya uhakiki wa walengwa baada ya mafunzo hayo.

“Hakikisheni mnakuwa waadilifu mnapokwenda kufanya kazi ya uhakiki na kuhakikisha mnaondoa kaya zote ambazo zimepoteza sifa.”

 

Speratus Buberwa kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo alihaidi kufanya kazi ya uhakiki wa kaya za walegwa kwa kufuata miongozo waliyopewa  ili kupata walengwa wenye sifa zilizokusudiwa na mradi.  

Baada ya kukamilika Kipindi cha Kwanza,  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliamua kuendelea na Kipindi cha Pili katika Awamu ya Tatu ya TASAF  ili kaya zote zinazoishi katika mazingira duni zipate usaidizi wa Serikali kupitia TASAF kwa kuwawezesha kufanya kazi na kupambana na umaskini.


 

 Afisa Ufuatiliaji TASAF Makao Makuu  Moris Momba akitoa mafunzo ya namna ya kutumia Kishikwambi wakati wa uhakiki wa  Walengwa.


Baadhi ya washiriki wa mafunzo.



Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa