• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WiLDAF Tunaomba mtanue eneo la Mradi

Imewekwa: March 13th, 2021

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe Paul Cheyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bukombe ameliomba shilika lisilo kiserikali la WiLDAF (Womem in Law and Development in Africa) kuhakikisha linaongeza eneo la mradi kwa maeneo yaliyobakia.

"Tunaomba mtanue eneo la mradi  ili kata zote ziweze kufikiwa na wanawake wa Bukombe waweze kufikia hamsini kwa hamsini katika nafasi za uongozi"

Cheyo ameyasema hayo tarehe 13 Machi, 2021 wakati wa mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Wilayani Bukombe  yaliyofanywa na shirika la WiLDAF kupitia mradi wake wa Wanawake Sasa yenye Kauli Mbiu isemayo "Wanawake katika Uongozi: Chachu Kufikia Dunia yenye Usawa."

Akitoa salamu za ufungunzi wa maadhimisho hayo Afisa Program Mwandamizi Agnes Mtuhi amesema kupitia mradi wa Wanawake Sasa wanawake wengi walijitokeza  kushiriki katika uchaguzi wa mwaka 2020 na kufanikiwa kushika nyadhifa mbalimbali kama ubunge, udiwani na uwakilishi katika mabalaza ya vijiji, kitu ambacho kilikuwa adimu sana kwa miaka ya nyuma.

Aidha aliendelea kusema kuwa ushiriki wa mwanamke katika uongozi unakabiliwa na changamoyo nyingi zikiwemo mila na mtazamo potofu, ukatili wa kijinsia, sheria zenye mapungufu, ukosefu wa fedha, kutojua taratibu za kufuata hasa wakati wa kujiunga na vyama vya siasa na chaguzi ndani ya vyama na jamii kutotoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi wanawake.

Agnes Mtuhi Afisa Program Mwandamizi WiLDAF.

Naye Mratibu wa mradi wa Wanawake  Sasa Wilaya ya Bukombe Mariana Genya amesema mradi wa Wanawake Sasa  umefanikiwa kufikia wadau mbalimbali ambao ni Kikundi cha Mwanamke Sasa wadau wao wakiwa ni AMCOS, Bodaboda na wasaidizi wa sheria, Viongozi wa kimila, Viongozi wa dini, waandishi wa habari na vikundi vya ngoma za asili ambao tuliona wanaweza kutoa nafunzo kwa jamii kuhusu masuala ya kijinsia kupitia sanaa.

Aidha Shirika la WiLDAF kuanzia tarehe 11 - 12 Machi, 2021 lilitoa mafunzo juu ya ukatili dhidi  ya wanawake kwenye siasa kwa kikundi cha Wanawake Sasa pamoja na Wajumbe wa Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ( MTAKUWA) lengo likiwa ni kupata elimu ya kutosha katika maswala ya uongozi na usawa wa kijinsia na kuleta maendeleo yanayozingatia usawa katika jamii ya Bukombe.

Idd Rajabu Mzirai Mwezeshaji wa mafunzo kutoka shirika la WiLDAF akifundisha baadhi ya washiriki wa mafunzo.

Shirika la WiLDAF(Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika) kupitia Mradi wake wa Wanawake Sasa ulizinduliwa mwaka 2019 Wilayani Bukombe likiwa na lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi kupitia uhamasishaji jamii. Mradi huu ilianza na kata 5 ambazo ni Namonge,Uyovu, Bulega, Katente na Bukombe na sasa zimeongeza kata zingine 2 na kupelekea kuwa na jumla ya kata 7 ambazo ni Igulwa na Bulangwa.


Baadhi ya viongozi walioshiriki mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 2021.


Baadhi ya Wanawake walioshiriki Sherehe za maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.









Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa